Ticker

6/recent/ticker-posts

Moto kati ya Mbunge na wananchi wake

 Raisa Said , Korogwe



Wananchi wa wilaya ya Korogwe wametahadharishwa juu ya athari za kutozingatia maelekezo ya wataalamu wa Afya yanayohusiana na Elimu ya Afya ya Uzazi hususani ujauzito na kujifungua kwa wanawake wanaobeba Ujauzito wa Kwanza na wale wanaobeba ujauzito katika Umri mdogo


Tahadhari hiyo imetolewa na Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mzava

mara baada ya kufika Kijiji Cha Kizara na kufuatilia msichana mmoja

mwenye umri wa miaka 15 kupoteza mtoto baada ya kucheleweshwa

kupelekwa kwenda kituo cha afya kilichopo Magoma. .



Mbunge huyo alisema kuwa kama binti huyo angepelekwa katika kituo cha

afya kama alivyoelekezwa na wahudumu wa Zahanati ya kijijini hapo

inayohudumia vijiji vitano vilivyopo katika kata hiyo na kata za

jirani. asingepoteza mtoto wake.


“Inashangaza kuona msichana huyo alipewa ushauri kwenda

kujifungua kituo cha afya Magoma lakini wazazi walipuuza ushauri huo

na kusababisha binti huyo kupoteza mtoto wake. Huo ni uzembe,” alisema

Mbunge huyo.


Mnzava aliwataka wnanachi kuzingatia maelekezo ya elimu ya afya

yanayoyotolewa na wataalam wa afya ili kuondoa matatizo na changamoto

mbalimbali zinazoweza kujitokeza.


Awali Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Vijijini, Miriam Cheche alisema

kuwa maeleze aliyopewa baada ya kufuatilia tatizo hilo aliambiwa na

binti huyo kuwa walipewa ushauri katika zahanati ya kijiji hicho wa

kwenda katika kituo cha afya cha Magoma kwa ajili ya kujifungus kwa

mujibu wa maelekezo ya kitaalamu .


Mganga huyo Mkuu alisema kuwa binti huyo alieleza kuwa Baba yake

alisisitiza apelekwe katika kituo cha afya lakini mama yake alikataa

na kusema kuwa atajifungulia nyumbani ambako alidai kuna wakunga

watakaomzalisha


“wangezingatia ushauri binti huyo asingetepoteza mtoto. Hata

angekwenda katika zahanati hiyo ya kijiji anageambiwa aende katika

kituo cha afya,” alisema Mganga Mkuu huyo.



Dk Miriam Cheche alisema kuwa hata hivyo Halmashauri hiyo inakabiliwa na

upungufu mkubwa wa watumishi wa afya ambayo inalazimika kusambaza

watumishi hao wawili kila zahanati.


Alieleza kuwa kuna vituo vya afya 49 ambavyo katika hivyo kuna

Hospitali moja na vituo na vituo vine vya afya. Alieleza sehemu za

huduma ya afya zitaongezeka kufikia 55 kutokana na kuwepo kwa maboma

6 ambayo yatakamilishwa kwa fedha zilizotolewa na serikali.



Kuhusu watumishi alisema kuwa sasa hivi wapo 270 na wameletewa wengine

43 ambao alisema bado ni kidogo kutokana na mahitaji. “Tunahitaji kuwa

na watumishi angalau 10 kila kituoa cha afya au zahanati ili kutoa

huduma ya kuridhisha.. aliwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati

serikali inatatua tatizo la upungufu wa watumishi.


Mama mmoja Tatu Kasimu, Mkazi wa kijiji hicho aliiomba serikali iweke

kktuo cha afya hapo Kizara ili kuokoa kuondoa mateso ya wagonjwa ambao

wanalazimika kusafiti mwendo mrefu kwenda Magoma.


Mwingine Asia Abdalla Shewali Mhina alisema kuwa kila siku watu

wanapata elimu kuwa mimba ya kwanza wanataliwa kwenda katika kituoa

cha afya. “ Kila siku Tunapewa somo kuwa mimba ya kwanza nay a

kuendelea inabidi kwenda kuzalia katika kituoa cha afya. Kwa hiyo kama

ni kosa ni kosa lao wenyewe. Nesi hana kosa,” alisema.


Mbunge huyo ameanza ziara ya siku sita katika Jimbo lake Hilo.




Post a Comment

0 Comments