Ticker

6/recent/ticker-posts

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

 SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.


Saikolojia ni nini?


Neno kuu linalobeba dhana ya saikolojia ni tabia. Tunapozungumzia tabia, tuna maana ya matendo, miitikio au mienendo inayoweza kuonekana wazi, kupimwa na hata kuchunguzika kwa kufuata misingi ya kisayansi. Kwa maana hiyo, saikolojia ni sayansi ya kuchunguza tabia, mitazamo, imani walizonazo watu na namna inavyoathiri wayatendayo.


Upo uhusiano wa karibu kati ya mitazamo na imani zisizoonekana na tabia inayoonekana. Hasira ni tabia kwa sababu kwanza, ni kitendo kinachoweza kuonekana bayana kwa macho kupitia yanayofanywa na mwenye hasira, na hivyo inaweza kupimwa kisayansi kwa kufuatilia vitendo vinavyoonesha hasira ili kuweza kufanyiwa utafiti unaokubalika. Maelezo hayo hayo yanaweza kutumika kuelezea tabia yoyote kama vile kupenda, kunyanyapaa na kadhalika kwa sababu, vyote kwa pamoja, vinaonekana, vinapimika na vinachunguzika kwa kufuata kanuni za kisayansi.



Post a Comment

0 Comments